Nchi jirani na DRC zatakiwa kuchukua hatua kukabiliana na EbolaNchi jirani na DRC zatakiwa kuchukua hatua kukabiliana na Ebola

Shirika la afya duniani WHO limeonya kwamba mataifa Jirani na nchi ya DRC yanakabiliwa na hatari kubwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Ebola, na yanapaswa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na virusi hivyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imetolewa na mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye alitangaza pia ziara yake siku ya Jumanne nchini DRC ambayo ni kitovu cha mlipuko mpya wa virusi hatari vya Ebola.

Tedros aliiabia kikao cha mawaziri kilichofanyika kupitia njia ya mtandaoni, kwamba virusi hivyo vinasambaa kwa kasi na kwamba mlipuko wa sasa unakumbwa na changamoto kubwa.

Wahudumu wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakiwa katika hospitali kuu Rwampara katika Mji wa Bunia jiji Ituri.
Wahudumu wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakiwa katika hospitali kuu Rwampara katika Mji wa Bunia jiji Ituri. REUTERS – Gradel Muyisa Mumbere

Mbali na changamoto ya kuchelewa kugundua virusi hivyo, hali inayofanya kuwa vigumu kukabili janga hilo, Tedros alitaja ukosefu wa usalama katika maeneo ya mashariki mwa DRC pamoja na ukosefu wa imani kati ya wakazi wa eneo hilo na mamlaka  kutoka nje.

Adiha Tedros pia alibainisha ukosefu wa chanjo ilioidhinishwa kwa ajili ya aina ya virusi hivyo vya Bundibugyo kama chanzo cha mlipuko unaoshuhudiwa.

Jumamosi iliopita, kituo cha kudhibiti magonjwa Afrika CDC kilisema nchi kumi ziko katika hatari ya kukumbwa na mlipuko huo, nchi hizo ni pamoja na  Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Congo, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Zambia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *