
Marekani inasema wnanajeshi wake wametekeleza mashambulio mapywa, Kusini mwa Iran kulenga vituo vyake vya makombora na boti zinazotumiwa kutega vilipuzi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jeshi la Marekani limesema, licha ya kuwepo kwa mkataba wa usitishwaji vita, mashambulizi hayo yametekelezwa ili kujilinda.
Aidha,Marekani inasema, mashambulizi hayo yalilenga pia kuwalinda wanajeshi wake dhidi ya hatari iliyopo kutoka kwa vikosi vya Iran.
Msemaji wa Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani Kaptain Tim Hawkins, amesema vikosi vya Marekani vitaendelea kujilinda licha ya kuwepo kwa mkataba wa kusitisha vita, wakati huu mazungumzo yakiendelea.
Mashambulizi haya yamekuja, wakati msemaji wa Mambo ya nje wa Iran Esmail Baqai, akisema hatua kubwa imepigwa kwenye mazungumzo na Marekani, lakini hakuna matumaini ya kupata mkataba wa kumaliza vita hivyo kwa sasa.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio siku ya Jumanne, amesema bado kuna uwekezano wa kupatikana kwa mkataba huo, huku wajumbe wa Iran wakiwasili Doha kwa ajili ya awamu nyingine ya mazungumzo.
