Afrika Kusini: Serikali yasema inashugulikia suala la raia wa kigeniAfrika Kusini: Serikali yasema inashugulikia suala la raia wa kigeni

Serikali ya Afrika Kusini inasema, inashughulikia suala la kuwepo kwa raia wa kigeni wanaoishi nchini humo bila vibali, ikiwataka raia wa nchi hiyo kutochukua hatua mikononi mwao.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya serikali inakuja wakati huu maandamano dhidi ya wageni wanaoishi nchini humo bila vibali, yakiendelea kwenye miji mbalimbali.

Mawaziri mbalimbali wamekutana kwenye kikao cha dharura kujadili madai kuwa wageni wasio na vibali, wanasababisha visa vya utovu wa usalama nchini humo na kuchukua ajira za wenyeji.

Ghana kuwaondoa raia wake 300 kutoka nchini Afrika Kusini.
Ghana kuwaondoa raia wake 300 kutoka nchini Afrika Kusini. Reuters – Siphiwe Sibeko

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Njabulo Nzuza amesema, Afrika Kusini inakabiliwa na changamoto kubwa ya wahamiaji haramu na inataka mchakato wa kuwaondoa nchini humo ufuate sheria.

Hii inakuja baada ya wiki iliyopita, mamia ya raia wa kigeni kutoka mataifa kama DRC, Rwanda na Somalia kutafuta hifadhi kwenye mji wa Durban baada ya kupokea vitisho kutoka kwa wenyeji kuwa, kufikia Juni tarehe 30 wawe wameondoka nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *