Barcelona yakaribia kumnasa Gordon, Rashford kikaangoniBarcelona yakaribia kumnasa Gordon, Rashford kikaangoni

Barcelona imefikia pazuri katika mpango wake wa kumnasa winga wa Newcastle United, Anthony Gordon baada ya leo Jumapili, Mei 27, 2028 kufanya makubaliano naye binafsi.

Inaripotiwa kwamba klabu hiyo na upande wa mchezaji wameafikiana juu ya maslahi yake binafsi na sasa inasubiriwa Newcastle United kuridhia ili nyota huyo atue kwa miamba hiyo ya Hispania.

Baada ya Gordon kuridhia kutua Barcelona, klabu hiyo tayari imeshawasilisha ofa ya Euro 70 milioni mezani kwa Newcastle United ambayo inasubiriwa kutoa majibu kama itaipokea au itahitaji zaidi ya kiasi hicho.

Ikiwa Barcelona itakamilisha uhamisho huo wa Gordon, hapana shaka itakuwa imeipa pigo Bayern Munich ambayo ilionekana kama ndio inakaribia kumnasa mchezaji huyo.

Gordon amekuwa na msimu bora katika kikosi cha Newcastle United kwenye msimu uliomalizika wa 2025/2026.

Gordon amefunga jumla ya mabao 17 katika mechi 41 za Newcastle United kwenye mashindano tofauti.

Kusajiliwa kwa Gordon kunaweza kuwa habari isiyovutia kwa winga wa Manchester United, Marcus Rashford ambaye amekuwa na mategemeo ya kusajiliwa moja kwa moja na Barcelona baada ya kuitumikia kwa mkopo katika msimu uliomalizika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *