Chanzo kimoja cha habari cha Pakistan kimeripoti kuhusu upinzani wa wazi wa Islamabad dhidi ya ombi la Rais Donald Trump wa Marekani la kuitaka nchi hiyo ijiunge na mchakato wa kurejesha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, na kuongeza kuwa Islamabad inaiona hatua ya Washington kuwa jaribio la kutumia vibaya diplomasia ya “kusimamisha vita na Iran” ili kutoa mashinikizo katika kesi zisizohusiana.
Swali ni kuwa je, kwa nini Trump anashinikiza kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala ghasibu wa Israel na Pakistan?
Pakistan ni mojawapo ya nchi muhimu na kubwa zaidi za Kiislamu, na bila shaka kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni kutakuwa na faida na maslahi makubwa kwa Tel Aviv. Mtazamo wa Donald Trump ni kwamba Pakistan ambayo hivi sasa ni mpatanishi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, inaweza kuishawishi nchi hii pia kuwa na uhusiano wa awaida na Israel na hivyo kuuletea utawala huo wa Kizayuni faida kubwa ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi.
Sababu nyingine ni kwamba licha ya kupita takriban miaka minne tangu kumalizika muhula wa Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa sasa wa utawala huo, hajafanikiwa kivyo vyote kupanua mapatano ya Abraham na wala hakuna nchi yoyote ya Kiislamu iliyoanzisha uhusiano wa kawaida na Israel katika miaka hii minne. Kuishawishi Pakistan ianzishe uhusiano na utawala wa Kizayuni kunaweza kufidia kushindwa huko kukubwa kwa Netanyahu. Sababu nyingine ni kuwa, utawala wa Kizayuni umekuwa miongoni mwa tawala zinazochukiwa zaidi duniani katika kipindi cha miaka 3 iliyopita kutokana na jinai za kutisha ulizofanya dhidi ya watu wa Gaza, Lebanon na Iran. Chuki hii ni kubwa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu kuliko maeneo mengine ya dunia. Sasa Trump anajaribu kuishawishi Pakistan iwe na uhusiano wa kawaida na utawala wa kibaguzi wa Israel, ili kujaribu kuonyesha kwamba kiwango cha hasira ya kimataifa dhidi yake kimepungua.
Sababu nyingine muhimu zaidi ni kwamba utawala ghasibu wa Israel unatarajiwa kuandaa uchaguzi wa bunge katika miezi michache ijayo, ambapo chama cha Likud kinachoongozwa na Netanyahu kinashuhudia mporomoko wa kisiasa miongoni mwa maghasibu wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Kwa kusukuma kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Pakistan na utawala wa Israel, Trump anajaribu kumuandalia njia

Netanyahu ili aweze kushinda uchaguzi ujao na hivyo kumbakisha katika nafasi hiyo ya waziri mku
Suala muhimu, hata hivyo, ni kwamba Pakistan haijakubali mashinikizo hayo na imekataa ombi hilo la Trump. Khawaja Muhammad Asif, Waziri wa Ulinzi wa Pakistan, amesema kuwa kujiunga na Mkataba wa Abraham kunakwenda kinyume na imani pamoja na fikra za kisiasa na kijamii za nchi hiyo, na kwamba Islamabad haitajiunga na makubaliano ambayo yanapingana na fikra za kimsingi za watu wa Pakistan. Amesisitiza kwamba yeye mwenyewe anaamini kuwa nchi hiyo isijiunge na makubaliano yoyote yanayokinzana na itikadi zake za kimsingi. Waziri wa Ulinzi wa Pakistan ameongeza kuwa jina la Israel halijaandikwa katika pasipoti za Pakistan na kwamba hiyo ndiyo nchi pekee iliyo na mtazamo wa aina hiyo.”
Upinzani wa Pakistan dhidi ya ombi hilo la Trump unawasilisha ujumbe muhimu kwamba chuki dhidi ya utawala wa Kizayuni iko katika kiwango cha juu hata miongoni mwa viongozi ambao wana uhusiano wa kirafiki na Marekani, na kwamba juhudi za Marekani za kupunguza chuki hiyo hazijafanikiwa. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kuchukiwa duniani utawala wa Kizayuni ni natija muhimu ya moja kwa moja ya jinai zake za kutisha na za mara kwa mara hususan katika miaka mitatu iliyopita, dhidi ya mataifa ya Asia Magharibi.
