Viongozi wa dini ya Kiislamu wametakiwa kuhakikisha vijana wanapewa kipaumbele katika kufundishwa maadili na misingi ya imani.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ally Ngeruko, wakati wa Baraza la Eid al-Adha kitaifa lililofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohammed VI uliopo makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Amesema ni muhimu kuandaliwa programu maalum zitakazowaweka vijana karibu na dini, huku akiwataka wazazi, licha ya majukumu yao, kutenga muda wa kuwa karibu na watoto wao ili kuwaongoza katika maadili mema.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)
