Al-Houthi: Umma wa Kiislamu unapaswa kujifunza kutokana na mapambano ya Iran dhidi ya Marekani na IsraelAl-Houthi: Umma wa Kiislamu unapaswa kujifunza kutokana na mapambano ya Iran dhidi ya Marekani na Israel

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa: Msimamo imara wa Iran unapaswa kuwa kichocheo cha kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

Sayyid Abdul Malik Badruddin al-Houthi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza umuhimu wa nafasi ya Iran katika Mhimili wa Muqawama na kusema: Msimamo imara wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya uchokozi wa Marekani na Israel ni somo kubwa kwa Umma Kiislamu, na kusimama kidete Tehran ni jambo muhimu katika kuimarisha undugu wa kikanda na ushirikiano ili kukabiliana na adui wa pamoja.

Akizungumzia matukio ya sasa huko Palestina na Lebanon, amesema kusimama imara na mapambano madhubuti ya Iran dhidi ya sera za kupenda makuu za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ni “somo kubwa kwa Umma wa Kiislamu.” Ameongeza kuwa: “Umma wa Kiislamu unapaswa kujifunza masomo muhimu kutokana na uimara na kusimama kidete kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na uchokozi wa Marekani na Israel.”

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Al-Houthi ameonya kuhusu matokeo mabaya ya kukaa kimya mbele ya vitendo viovu vya Wazayuni akisema: “Kupuuza majukumu yetu kuhusu Palestina kunafungua njia ya kupanuliwa uchokozi wa adui Mzayuni kwa lengo la “kubadilisha Mashariki ya Kati” na kuunda kile kinachoitwa “Israel Kubwa.”

Pia ameashiria uchokozi wa Wazayuni dhidi ya Lebanon na kuthamini utendaji wa uwanjani na wa kulipiza kisasi wa wapiganaji wa Hizbullah. Amesema: “Wapiganaji wa Hizbullah ya Lebanon wanakabiliana na mashine ya vita ya utawala wa Kizayuni kwa nguvu na ufanisi kamili, na muqawama huo umemzuia adui kufikia malengo yake mabaya katika eneo hilo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *