
Idara ya Mahusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kuwa: Kituo cha anga cha Marekani kilichotumiwa kufanya uchokozi dhidi ya Bandar Abbas kusini mwa Iran, kimelengwa alfajiri ya leo Alkhamisi saa 10:50.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema: Kufuatia shambulio la alfajiri siku ya Alhamisi la jeshi wavamizi la Marekani nje kidogo ya uwanja wa ndege wa Bandar Abbas lililofanyika kwa kutumia makombora ya anga, kituo cha anga cha Marekani kilichotumiwa kufanya uchokozi huo, kimelengwa shabaha saa 10:50 alfajiri.
Taarifa ya Idara ta Uhusiano wa Umma ya IRGC imesema: “Jibu hili ni onyo zito ili adui ajue kwamba uchokozi wa aina yoyote hautapita biila kujibiwa, na ikiwa utarudiwa, jibu letu litakuwa kali zaidi.”
Taarifa hiyo inakuja baada ya Jeshi la Wanamaji la IRGC siku ya Alhamisi kulazimisha meli ya mafuta ya Marekani kurudi nyuma. Meli hiyo ilikuwa ikijaribu kuvuka kinyume cha sheria Mlango-Bahari wa Hormuz baada ya kuzima mfumo wake wa ufuatiliaji, licha ya vikwazo vya Iran.
Iran ilifunga Mlango-Bahari wa Hormuz kwa maadui na washirika wao baada ya mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani na utawala wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, mnamo Februari 28.
