Kundi la kwanza la Waghana lawasili Accra baada ya kurejeshwa kutoka Afrika KusiniKundi la kwanza la Waghana lawasili Accra baada ya kurejeshwa kutoka Afrika Kusini

Kundi la kwanza la karibu Waghana 300 waliorudishwa kutoka Afrika Kusini kutokana na hujuma za kupinga wahamiaji, liliwasili Accra jana Jumatano.

Waghana hao walikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Samuel Okudzeto Ablakwa, huku nyimbo za kizalendo zikipigwa katika uwanja wa ndege.

Karibu Waghana 800 wamejiandikisha kwenye ofisi ya ubalozi wa nchi hiyo kwa ajili ya safari za ndege za kurudi nyumbani wakisema hawajisikii salama tena nchini Afrika Kusini.

Accra imetayarisha safari hizo kujibu wimbi la maandamano na vurugu zinazowalenga wageni wasio na wenye vibali rasmi vya kuishi nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini, uchumi ulioendelea zaidi katika bara la Afrika, kwa muda mrefu imekuwa kivutio cha wafanyakazi halali na wasio na vibali.

Haya yanakuja wakati ambapo Afrika Kusini, uchumi mkubwa zaidi wa viwanda barani Afrika, inakabiliwa na mashinikizo ya kijamii yanayoongezeka kutokana na ukosefu wa ajira wa karibu 30%, jambo ambalo limechangia kuongezeka chuki dhidi ya wahamiaji na katika baadhi ya matukio, vurugu na machafuko.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa idadi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini inazidi milioni tatu, ikiwa ni takriban asilimia 5.1 ya idadi ya watu. Wengi kati ya wageni hao wanatoka nchi jirani ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

 Awali, Serikali ya Ghana ilisema zoezi la kuwarejesha nyumbani raia wa nchi hiyo walioko huko Afrika Kusini linalenga kuhakikisha usalama na ustawi wa raia huku kukiwa na ongezeko la mvutano na mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *