Nigeria: Atiku Abubakar kuwania urais kwa tiketi ya ADCNigeria: Atiku Abubakar kuwania urais kwa tiketi ya ADC

Nchini Nigeria, kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Januari mwaka ujao, vyama vya siasa tangu Mei tarehe 23 vimekuwa vikifanya uchaguzi wa ndani, kuwachagua wagombea urais na nyadhifa zingine za uongozi kama wagombea wa Ugavana na Maseneta.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jumamosi Mei tarehe 30 ndio siku ya mwisho wa uchaguzi huo ndani ya vyama, kwa mujibu wa Kalenda iliyotangazwa na Tume ya uchaguzi.

Tayari chama tawala APC (All Progressives Congress), kimemteua rais Bola Tinubu kuwania tena uongozi wa nchi hiyo kwa muhula wa pili.

Kuendelea kwa uchaguzi huu ndani ya vyama, umedhirisha namna vyama vya upinzani vilivyogawanyika, kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Siku ya Jumatano chama cha ADC (African Democratic Congress) kilimteua aliyewahi kuwa Makamu wa rais Atiku Abubakar, licha ya kupingwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho.

Vyama vingine vya upinzani vinavyoendelea na zoezi hili ni pamoja na chama cha PDP kilichowahi kushika madaraka huko nyuma na kile cha NDC.

Chama cha PDP kinashuhudia mpasuko, kuna wale wanaomuunga mkono aliyewahi kuwa rais Goodluck Jonathan kuwa mgombea wake, lakini kuna kundi lingine linalomtaka mwanasiasa Sandi Onor kupeperusha bendera ya chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *