‘Sikukuu ya wanyonya damu imekwisha’: Iran yasema hakuna ngao tena kwa kambi za Marekani‘Sikukuu ya wanyonya damu imekwisha’: Iran yasema hakuna ngao tena kwa kambi za Marekani

Ulinzi wenye nguvu wa Iran umeonyesha kwamba “sikukuu ya wanyonya damu” imekwisha.

Hayo ni matamshi ya afisa mkuu wa usalama wa Iran katika mkutano wa usalama huko Moscow, ambapo ameeleza maono ya Tehran ya usanifu mpya wa usalama eneo la Asia Magharibi kufuatia vita vya siku 40 na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Ali Bagheri, Naibu Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC), amewahutubia wawakilishi wakuu wa usalama kutoka zaidi ya nchi 120 katika Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Maafisa wa Usalama wa Vyeo vya Juu katika mji mkuu wa Russia, Moscow.

Bagheri alifungua hotuba yake kwa kusema kwamba taifa la Iran kwa sasa liko katika “vita vikali vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa Kizayuni” – vita vilivyosababisha kuuawa shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na makatibu wawili mfululizo wa Usalama wa Taifa (SNSC), Admiral Ali Shamkhani na Dkt. Ali Larijani.

Vilevile ameashiria shambulio la makusudi dhidi ya shule Msingi ya Minab, ambapo watoto 168 waliuawa shahidi, akisema ukatili huo ulikusudiwa kulazimisha taifa la Iran lijisalimishe.

“Lakini ustahimilivu wa kushangaza wa watu wa Iran na vikosi vyetu vya kishujaa ulithibitisha kwamba matarajio, hesabu na mifumo ya kijeshi ya adui ilishindwa kwa wakati mmoja dhidi ya uwezo na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,” amesema.

Bagheri amesema kwamba dunia sasa iko katika njia panda ya kihistoria. “Kwa upande mmoja, Kusini na Mashariki ya Dunia wanaelekea kwenye ushirikiano wa pande kadhaa; na kwa upande mwingine, nchi za Magharibi zenye ukatili, zinazoogopa kupungua na kuanguka misingi yao ya nguvu ya kikoloni, zimeweka sera ya matumizi ya nguvu kali na kijeshi katika ajenda yake.”

Ameongeza kuwa: “Chaguo la dunia ni ushirikiano, kupinga dunia ya kambi moja na kukataa utawala wa kibeberu.”

Bagheri amekitaja kile kinachoitwa Makubaliano ya Abraham (Abraham Accords)- makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida baina ya nchi za Kiarabu na Israel yanayoungwa mkono na Marekani – kuwa ni “Makubaliano ya Firauni”.

“Jina halisi la mpango huu si Makubaliano ya Ibrahimu – ni Makubaliano ya Farauni,” amesema Naibu Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran na kuongeza: “Utawala wa Kizayuni ni Farauni wa sasa, anayetaka kutawala eneo la Asia Magharibi kupitia mauaji ya watoto na uchokozi. Makubaliano ya Farauni yanalenga kuzifanya serikali na mataifa ya eneo hilo kuwa watumwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *