Mshauri wa Ndoa na Maendeleo ya Kazi kwa Vijana, Angela Mutashobya, amesema ndoa nyingi za vijana kwa sasa zinakabiliwa na changamoto kubwa zinazochangiwa na athari za utandawazi na kasi ya mabadiliko ya maisha ya kisasa.

Amesema vijana wengi wamekuwa wakitoa kipaumbele kwa mitindo ya maisha wanayoiona kupitia mitandao na majukwaa mbalimbali ya kidijitali kuliko kuzingatia hali halisi ya maisha yao, jambo linalowafanya kufanya maamuzi ya haraka bila kuyatafakari kwa kina. Hali hiyo, kwa mujibu wake, imechangia ndoa nyingi za vijana kutodumu kwa muda mrefu.

✍Ibrahimu Kilumbo
Mhariri | @rajmsangi
@mercy.mbaya
@david_wakarungi

#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *