Watu hawa wanne ambao walitibiwa kwa mchanganyiko wa viuavijasumu na dawa zingine kana kwamba walikuwa wakiugua malaria, wamefanikiwa kupona ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo na wanawakilisha matumaini katika mapambano dhidi ya aina hiyo ambayo bado hakuna chanjo wala tiba, amesema mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ambaye waliwasilishwa kwake.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Pascal Mulegwa

Ingawa virusi hivi vua Ebola aina ya Bundibugyo inayoenea mashariki mwa DRC bado haina chanjo wala tiba, hata hivyo kuna ishara ndogo ya matumaini katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Huko Bunia, katika mkoa wa Ituri, watu wanne walioambukizwa virusi hivyo wamepona , na kufanya jumla ya idadi ya waliopona ugonjwa huo hatari kufikia watano.

Wagonjwa wote wanne, ambao ni wafanyakazi wa afya, waliwasilishwa kwa mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Ghebreyesus, ambaye bado anazuru nchi hiyo.

Picha zilizopigwa katika Kituo cha Matibabu cha Kiinjili huko Bunia, zilizoshirikiwa na Wizara ya Afya ya Kongo, zinaonyesha muuguzi akisimulia mateso yake. “Ebola ni ugonjwa mbaya, niliteseka,” anasema. “Leo, nashukuru kwa sababu nimepona, lakini bado ninasumbuliwa na hasara zilizonizunguka. Kwa mfano, daktari wangu aliyenihudumia alifariki. Mwanzoni, hatukushuku chochote, na, kama wengine wengi, tuliambukizwa kwa kuwahudumia wagonjwa bila kinga,” alisema.

“Nyinyi ni uthibitisho hai kwamba mlipuko huu unaweza kudhibitiwa.” Mtaalamu wa tiba ya viungo Mika pia anasimulia jinsi alivyougua ugonjwa huo hatari. “Nililazwa hospitalini kwa siku 10 kuanzia Mei 16.” “Nilipata huduma na matibabu ya kliniki ambayo yalinifaa. Nimepona,” alisema.

Akiwahutubia, Tedros Gebreyesus alionyesha kuridhika kwake na ishara za kutia moyo ambazo kupona kwao kunatuma katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. “Ujasiri wenu unatoa matumaini kwa sababu ni uthibitisho hai kwamba janga hili linaweza kudhibitiwa,” aliwaambia kabla ya kuwashukuru tena wafanyakazi wa afya kwa kujitolea kwao. “Ninajua huu ni wakati hatari sana kwenu, na inaniuma kuona wahudumu wa afya wakifariki kutokana na Ebola wakati wakiwahudumia wengine. Kwa kweli mnahatarisha maisha yenu ili kuwasaidia wengine kuishi,” alibainisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *