Kombe la Dunia la mwaka 2026 linatarajiwa kuleta mabadiliko kadhaa katika sheria za mchezo (Laws of the Game) zitakazobadilisha namna soka linavyochezwa na kusimamiwa. Mabadiliko hayo yanalenga kupunguza upotevu wa muda, kuongeza haki katika maamuzi ya waamuzi na kudhibiti mbinu ambazo zimekuwa zikitumika kuvuruga kasi ya mchezo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi wa FIFA, Pierluigi Collina, amesema baadhi ya mabadiliko hayo tayari yameidhinishwa, huku mengine yakitarajiwa kutumika rasmi wakati wa mashindano hayo makubwa zaidi ya soka duniani. Lengo kuu ni kuhakikisha mchezo unakuwa wa kasi zaidi na wenye uwazi, huku matokeo yakiamuliwa zaidi na uwezo wa timu uwanjani.
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na malalamiko kuhusu mbinu za kupoteza muda na “mapumziko ya kimkakati” wakati wa mechi, ambapo baadhi ya wachezaji hujifanya kuumia ili kutoa nafasi kwa makocha kutoa maelekezo. FIFA sasa inachukua hatua kali kuhakikisha tabia hizo zinadhibitiwa.
Mabadiliko haya yanatarajiwa kuifanya Kombe la Dunia la 2026 kuwa moja ya michuano yenye sheria zilizobadilishwa zaidi katika historia ya soka la kisasa, huku waamuzi wakipewa mamlaka zaidi ya kusimamia mchezo kwa haki na kwa kasi.
#StadTv Update

(Feed generated with FetchRSS)