Kwa miaka mingi, picha ya kijana wa Kimasai akiwa amebeba fimbo, rungu au silaha za jadi imeendelea kuwa sehemu ya utambulisho wa jamii hiyo. Hata hivyo, katika Tanzania ya sasa ambako masuala ya sheria na usalama wa raia yamepewa kipaumbele zaidi, mjadala unaibuka kuhusu nafasi ya silaha hizo katika jamii.

Sawali linalojitokeza ni iwapo silaha hizo zinapaswa kuendelea kutazamwa kama sehemu ya utamaduni wa jadi au zinahitaji kuangaliwa upya kwa mujibu wa sheria na mazingira ya sasa ya usalama wa wananchi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *