.

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais Donald
Trump wa Marekani ameomba marekebisho yafanywe kwenye makubaliano kati ya
Marekani na Iran yanayolenga kukomesha mapigano yaliyoanza mapema mwaka huu,
vyombo vya habari vya Marekani viliripoti.

Mabadiliko
hayo yanahusiana na Mlango-Bahari wa Hormuz na kuondolewa kwa madini ya urani,
CBS News, mshirika wa habari wa BBC nchini Marekani, iliripoti. Ikulu ya White
House haikujibu ombi la kutoa maoni.

Mohammad
Bagher Ghalibaf, mpatanishi mkuu wa Iran, alisema Jumapili kwamba Tehran
haitakubali makubaliano yoyote isipokuwa haki za Iran zipatikane kikamilifu.

Rais na
wasaidizi wake wakuu walikutana Ijumaa kufanya “uamuzi wa mwisho” juu
ya mfumo wa kuongeza muda katika suala la kusitisha mapigano na Iran, lakini
mkutano huo ulimalizika bila ufafanuzi kuhusu hatua zinazofuata.

Makubaliano
hayo yaliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na Axios siku ya Jumamosi, yanajumuisha
kusitishwa kwa vurugu kwa siku 60, wito wa kufungua tena Mlango-Bahari wa
Hormuz na mfumo wa kufungua tena na mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa
Iran, kulingana na CBS.

Ikiwa
diplomasia itaendelea, makubaliano hayo pia yanaripotiwa kuhusisha uwezekano wa
kupunguzwa vikwazo kwa Iran ambavyo vinaweza kuiruhusu kupata mabilioni ya dola
katika mali zilizozuiliwa, CBS ilisema.

Ripoti za
Jumapili za marekebisho zaidi ni hatua ya hivi karibuni katika mazungumzo ya
siku nyingi kati ya Ikulu ya White House na Iran kuhusu mfumo wa makubaliano
yanayolenga kukomesha vita vya miezi kadhaa.

Siku ya
Alhamisi, maafisa wa Marekani walisema nchi hizo mbili zimekubaliana kuhusu
mfumo – unaojulikana kama mkataba wa makubaliano – unaosubiri idhini ya Trump
na uongozi wa Iran.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *