#HABARI: Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amewataka wananchi wa Hanang’ mkoani Manyara kutokubali kushawishiwa kushiriki maandamano ya vurugu yanayoweza kusababisha uharibifu wa mali za umma.

Akizungumza na wananchi wa Hanang’, Kihongosi alisema wanaochochea vurugu hawana maslahi ya wananchi, kwani madhara ya kuchoma vituo vya polisi, vituo vya afya na miundombinu mingine huwakumba wananchi wenyewe.

Alisisitiza kuwa “maandamano ya maendeleo” ni kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kipato na kuboresha maisha, akiwahimiza wakulima, wafanyabiashara na waendesha bodaboda kuzingatia shughuli zao za kiuchumi badala ya kushiriki vurugu.

Aidha, aliwataka wananchi kulinda amani na kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa manufaa ya familia na taifa kwa ujumla.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *