#HABARI: Rais wa Kenya, William Ruto, ametetea uamuzi wa Serikali ya Kenya kuruhusu kuanzishwa kwa kituo cha karantini ya Ebola katika kambi ya jeshi ya Laikipia Air Base, akisema hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama wa afya na ushirikiano wa Kimataifa katika kukabiliana na magonjwa hatari.
Rais Ruto alisema alitoa idhini ya mradi huo baada ya ombi kutoka kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, akisisitiza kuwa Kenya imekuwa mshirika muhimu katika masuala ya afya ya umma, udhibiti wa magonjwa na utafiti wa kitabibu.
Ruto ameeleza kuwa kituo hicho ni sehemu ya juhudi za kuimarisha utayari wa nchi dhidi ya mlipuko wa Ebola unaoendelea katika eneo la Afrika ya Kati, na kwamba Kenya tayari ina vituo vingine vya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza kote nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)