
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, hapo jana alitangaza kuunda serikali mpya iliyohusisha wandani wake na baadhi kutoka chama cha aliyekuwa waziri mkuu wake Osumane Sonko, ambaye amesema wanachama wake hawataingia kwenye baraza jipya la mawaziri.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye aliiteua serikali mpya Jumatatu, Juni 1 ambayo imewajumuisha baadhi ya wanachama na washirika wa Pastef, chama cha spika wa sasa wa Bunge la taifa Ousmane Sonko, licha ya tangazo la awali la Sonko kwamba chama chake hakitashiriki katika utawala mpya.
Sonko alitaja kutokubaliana kati yake na rais Faye kuhusu kile alichokitaja kuwa muundo wa baraza la watu hao haukubaliki.
Tangazo la serikali mpya linakuja siku 12 baada ya Rais Faye kumwondoa madarakani Ousmane Sonko kama waziri mkuu, ambapo siku mbili baadaye Sonko alichaguliwa na wabunge kuwa spika wa Bunge la Kitaifa.
Viongozi hao wawili wakuu walitengana baada ya miezi kadhaa ya mvutano, na kipindi cha kutokuwa na uhakika wa kisiasa nchini, kutokana na mgogoro mkubwa wa usimamizi wa fedha.