Chanzo cha picha, Reuters
Lebanon
inasema Hezbollah imekubali mpango wa Marekani wa kusimamisha mashambulizi
dhidi ya Israel na Israel isiushambulie mji mkuu wa Lebanon Beirut.
Ubalozi wa
Lebanon nchini Marekani ulisema “umepokea uthibitisho wa kukubali kwa
Hezbollah pendekezo la Marekani la kukomesha mashambulizi kwa pande zote
mbili”.
Waziri Mkuu
wa Israeli Benjamin Netanyahu alithibitisha makubaliano hayo, lakini alionya
kwamba mashambulizi dhidi ya Beirut yataendelea “ikiwa Hezbollah haitaacha
kushambulia miji yetu na raia”.
Taarifa hizo
zilikuja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema amezungumza na
wawakilishi wa Netanyahu na Hezbollah na “walikubaliana kwamba ufyatuaji
risasi wote utakoma”, baada ya Iran kuonya kwamba vitendo vya kijeshi vya
Israeli nchini Lebanon ni tishio kwa usitishaji mapigano wa sasa kati ya
Marekani na Iran.
Katika
taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni, ubalozi wa Lebanon ulisema kwamba “chini ya mpango uliopendekezwa, mashambulizi ya Israeli kwenye vitongoji
vya kusini mwa Beirut yatakoma badala ya Hezbollah kujizuia na mashambulizi
dhidi ya Israeli”. Iliongeza kuwa usitishaji mapigano “utaongezwa ili
kujumuisha eneo lote la Lebanon”.
Hata hivyo
Netanyahu alisema: “Wakati huo huo, IDF [Vikosi vya Ulinzi vya Israeli]
itaendelea kuendesha shughuli zake kusini mwa Lebanon kama ilivyopangwa.”
Baada ya
Trump kusema pande zote mbili zimekubaliana kuacha kupigana, mapigano mengine
yaliendelea.
Hezbollah
ilisema imeanzisha mashambulizi matatu dhidi ya vifaru na wanajeshi wa Israeli
karibu na vijiji viwili kaskazini mwa Israeli, ikitumia ndege zisizo na rubani
na “makombora ya mizinga”.
Soma zaidi: