Timu ya Taifa ya soka ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imeichapa Malawi goli moja kwa sifuri katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kalenda ya FIFA uliochezwa leo jioni uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Goli pekee la ushindi kwa Twiga Stars limefungwa na Mshambuliaji, Opah Clement.

Baada ya mchezo kumalizika Kocha wa Twiga Stars, Bakari Shime, amesema mechi mbili za kirafiki dhidi ya Malawi, moja ya leo na nyingine ya Juni 6 mwaka huu katika uwanja huo huo wa KMC Complex, zitamsaidia kuimarisha kikosi chake kimbinu na kiufundi kuelekea michezo ya ushindani.

Mhariri | @rajjmsangi
#Mshikemshike

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *