
Rais wa Urusi Vladimir Putin leo Ijumaa Juni 5, amepuuzia mbali ugumu wa kiuchumi unaoikabili nchi yake, katika jukwaa kubwa la uwekezaji huko St. Petersburg, akipendelea kusifu “uhuru” wake na ushirikiano wake na nchi za Kusini mwa Dunia.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Kutoka pande zote, tunaambiwa kwamba kila kitu kinaenda vibaya hapa (…). Ndiyo, kasi ya kiuchumi kwa sasa ni ya wastani,” Vladimir Putin ametangaza katika hotuba kwa maafisa wa Urusi na wa kigeni na viongozi wa biashara. “Katika muktadha tatanishi na mgumu, Urusi inaendelea kuimarisha uhuru wake (…) kwa kupanua kundi lake la washirika,” ameongeza.
Hata hivyo Urusi imeshuhudia kupanda kwa bei za bidhaa, nyongeza ya kodi, upungufu wa nafasi za kazi na kufungwa kwa biashara.
Jukwaa hilo la mwaka huwaleta pamoja wafanyabiashara na wawekezaji kutoka mataifa mengi duniani kwa majadiliano kuhusu uchumi na kutiliana saini mikataba ya kibiashara.