
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ameeleza kuwa mauaji ya Minab ni kati ya mamia ya jinai za Marekani na Israel dhidi ya Wairani.
Akihutubia kwenye hafla iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad kwa ajili ya kuwaenzi mashahidi wa shule ya Minab katika mkoa wa Hormuzgan kusini mwa Iran , Ismail Baqaei amesema: Kuheshimu kumbukumbu za watoto hao sio tu ni kuenzi tukio lililopita, bali ni wajibu wa kulinda ukweli, haki na ubinadamu, na mustakbali wa baadaye.
“Watoto ni wahanga wakubwa wasio na hatia na wa kwanza wa vita vyovyote; iwe ni wale wanaolengwa kwa risasi, mabomu na makombora, wale ambao miili na roho zao zina majeraha ya kudumu, au wale wanaobeba mzigo mzito wa kupoteza baba, mama au wapendwa wao katika kipindi chote cha maisha yao,” ameongeza Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran.
Mtu anapowazungumzia watoto wa Minab, kwa hakika wanazungumza kuhusu utu wa binadamu, haki ya kila mtoto kuishi, kujifunza, kuwana ndoto, na kujenga mustakabali chanya kwao; haki ambayo haipaswi kukanyagwa kwa sababu ya tamaa mbaya.
Baqaei amebainisha kuwa kwa watoto wengi vita vinaendelea kwa miaka mingi ambapo watoto hao huishi katika maumivu ya kimwili, huishi katika ulemavu,wasiwasi, ndoto mbaya, na huzuni kubwa ambayo hakuna dawa inayoweza kutibu.
Tarehe 28 Februari katika siku ya kwanza ya vita vyake vya kichokozi serikali ya Marekani ilikiuka sheria zote za kimataifa na kushambulia shule ya Msingi ya watoto wa kike ya Minab katika mkoa wa Hormuzgan (kusini mwa Iran) ambapo wanafunzi karibu 170 wa kike na walimu 20 wa shule hiyo waliuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa.