Nchi ya Rwanda, imeonya kile imesema upendeleo wa juhudi za Marekani katika upatanishi wa mgogoro wa mashariki mwa nchi ya DRC, kauli inayotolewa wakati huu Washington ikijaribu kuhakikisha mkataba wa amani uliotiwa Saini mwaka uliipita, unatekelezwa na pande zote.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Rwanda imekuja saa chache kupita baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio, kuwasilisha ripoti kwenye bunge la Seneti na kusema Kigali imeendelea kuheshimu na kutekeleza makubaliano ya Washington.

Kwenye taarifa yake, Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, amesema nchi yake itaendelea kuheshimu makubaliano yaliyofanikishwa na Marekani, lakini akasisitiza kuwa pande zote lazima ziwajibike kwa usawa.

Kigali inasema mkataba wa amani uliopo hauwezi kutekelezwa kwa upendeleo na kuonya kuwa mzozo wa mashariki mwa Congo hauwezi kutatuliwa kwa kile ilichokitaja kama upande mmoja.

Rwanda kwenye taarifa yake imesema kuwa, wakati ikiendelea kutimiza wajibu wake chini ya makubaliano iliyotia Saini, Serikali ya DRC imeendelea kuwaunga mkono wapiganaji wa FDLR, wanaotuhumiwa kuchochea vurudu dhidi ya Watusi wakati wa mauaji ya Kimbariy a mwaka 1994.

Marekani imekuwa ikiongoza juhudi za kidiplomasia kupunguza joto la mvutano kati ya Rwanda na DRC, lakini tangu kutiwa Saini kwa makubaliano mwezi Desembam waka jana, mapigano kati jeshi la Congo na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda, yameendelea kuripotiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *