
Jeshi la Israeli limetekeleza mashambulio mazito kulenga kambi za kijeshi Magharibi na eneo la Kati nchini Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Haya ni mashambulzi ya kwanza ya Israeli nchini Iran tangu mwezi Aprili, baada ya mkataba wa usitishwaji vita kati ya Iran, Marekani na Israeli.
Jeshi la Israeli kupitia kupitia ujumbe uliochapishwa kwenye ukurasa wake wa Telegram, limesema vikosi vyake vimesambulia miundo mbinu za kijeshi za utawala wa kigaidi wa Iran.
Iran nayo kupitia Televisheni ya taifa, imesema mashambulizi mazito yamesikika katika miji ya Tehran, Tabriz na Isfahan.
Israeli imetekeleza mashambulizi hayo, baada ya Iran kurusha makombora kuelekea Kaskazini mwa nchi hiyo, huku jeshi la kulinda mapinduzi ya nchi hiyi likitishia kuendelea mashambulizi hayo wiki hii. Hata hviyo, makombora ya Iran nchini Israeli,yameripotiwa kuzuiwa angani.
Rais wa Marekani Donald Trump ambaye amesema mashambulizi hayo hayatavunja mkataba wa kusitsha vita, ameripotiwa kuitaka Israeli kuacha kulipiza kisasi huku ikiiambia Israeli imetosha.