
Soko la kuweka miadi ya visa lina faida kubwa, lakini linamikanganyiko mingi kwa waombaji wanaolalamika kuhusu ugumu na gharama ya taratibu wa kuzipata.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwanahabari Sidy Yansané, alihusika alihusika katika uchunguzi na shirika la uandishi wa habari za uchunguzi Lighthouse Reports kampuni ambayo imekuwa muhusika mkubwa katika sekta hiyo, VFS Global, kampuni ya India ambayo serikali nyingi ulimwenguni zimekabidhi jukumu la kuchakachua maombi ya visa.
VFS Global inaripotiwa kupata faida kubwa kutokana na huduma hizi, hadi kufikia hatua ya kuvutia wadanganyifu…
Ndio VFS global inafanyakazi katika nchi 168, inamikataba na serikali 71.
Na wakati inaacha hali ya chungu kwa waombaji wa visa kutoka Afrika kama Aliou, msanii wa graffiti na mjasiriamali wa Senegal ambaye amezoea kuomba visa za kwenda Ulaya… Hivi majuzi alikataliwa, tena kwa sababu ya “mashaka” kuhusu kurudi kwake Senegal.
Kando na hasira hii inayoongezeka, vfs inapata faida kubwa.
Kulingana na taarifa za fedha za VFS Global zilizowasilishwa Luxembourg……faida yake ya uendeshaji imeongezeka mara nne katika kipindi cha muongo mmoja. Ambapo walifikia euro milioni 171 mwaka 2024… Na bado katika kipindi hicho hicho, idadi ya maombi ya visa iliongezeka kwa asilimia 15% tu……
Kampuni inaelezea ukuaji huu ni kutokana na uuzaji wa huduma za ongezeko la thamani,,,,, VAS……. kama vile habari kwa SMS au kufikia “eneo la VIP”…
Na ni huduma hizi zenye thamani iliyoongezwa vas ambazo ndizo kiini cha mkakati wa biashara wa kampuni.
Ndio, uchunguzi wetu unaonyesha kuwa VAS hizi zinawakilisha asilimia 30% ya mauzo ya kampuni duniani kote.
Nchini Afrika Kusini na Kenya, uuzaji wa huduma hizi unawakilisha zaidi ya theluthi moja ya mapato ya ndani ya VFS, zaidi ya robo nchini Nigeria.
Wafanyakazi wa VFS wamepewa mafunzo maalum ya uuzaji wa huduma hizi.
Wakiwa wamebanwa na usimamizi wao na pia wakichochewa na bonasi na kamisheni za mauzo, mawakala wa VFS hufichua kwamba huwatoza waombaji huduma hizi, bila kutaja kila mara kwamba hawakuwa wa lazima…. na, zaidi ya yote, kwamba hawahakikishiwi kabisa kupata visa.
Kwa mfumo huu, imeongezeka mitandao sanjari nje ya vfs kwenye mfumo huu.
Hawa ni wafanyakazi au waajiriwa wa zamani wa kampuni walioanzisha “wakala” haramu, wakipendekeza washirikiane na VFS na wahakikishe kupata visa, jambo ambalo ni uongo.
Lakini kutokana na kukata tamaa, waombaji wengi hukimbilia mashirika haya ya uwongo,,,, ambao wakati mwingine hutoza hadi euro 700 kwa huduma zao!
Na nini majibu ya vfs kwa yote unayoeleza kuhusu sera yake ya mauzo ya huduma… Au kwa kuwepo kwa mitandao ya ulaghai?
Ilipoulizwa kwa maandishi kwa ajili ya uchunguzi huo, VFS ilijibu kuwa “inatekeleza kwa vitendo hatua madhubuti za usalama”.
Na juu ya uuzaji wa huduma, kampuni inakumbusha “kwamba zinatengenezwa kwa makubaliano na serikali” na kwamba “imeonyeshwa wazi kuwa sio lazima” na juu ya yote kwamba hawana dhamana ya visa!