#HABARI: Zaidi ya watu 20,000 wamelazimika kuhama makazi yao kufuatia tetemeko kubwa lililotokea kusini mwa Ufilipino, ambalo pia limesababisha vifo vya watu 37.

Mamlaka za usimamizi wa maafa nchini humo zimesema kuwa uharibifu mkubwa wa nyumba na miundombinu umewalazimu wakazi wengi kuhama maeneo yao na kutafuta hifadhi salama.

Waokoaji wanaendelea kufanya kazi ya kutafuta watu ambao huwenda wamenaswa chini ya vifusi vya majengo yaliyobomoka, huku juhudi za misaada ya kibinadamu zikiendelea kuwafikia waathirika.

Serikali ya Ufilipino imesema inaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu na kuhakikisha msaada unawafikia wote walioathirika na janga hilo.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *