Katika ripoti iliyochapishwa leo Jumatano, Juni 10, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Watch linabaini kwamba Kigali na kundi AFC/M23 wamejihusisha na vitendo vilivyoainishwa kama uhalifu wa kivita katika kambi za kijeshi za Rumangabo na Tshanzu baada ya kutekwa kwa mji wa Goma mnamo Januari 2025. Ripoti hiyo pia inaishtumu Kinshasa, ambayo pia imetajwa kwa kuunga mkono makundi yenye silaha yanayohusika na unyanyasaji mkubwa. 

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Human Right Watch inabainisha kwamba Rwanda na mshirka wake AFC/M23 wanajihusisha na kuajiri watu wengi kwa nguvu, vipigo, upungufu wa maji mwilini, mauaji ya haraka…

Ripoti ya Human Rights Watch (HRW), iliyochapishwa leo Jumatano, Juni 10, inaituhumu AFC/M23 na jeshi la Rwanda kwa unyanyasaji mwingi, ambao wanauita uhalifu wa kivita, katika kambi mbili za kijeshi huko Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC.

Baada ya kukamatwa kwa jiji la Goma mnamo Januari 30, 2025, wakati malori 11 yalipoondoka Uwanja wa soka wa Unité yakiwa yamebeba takriban watu 1,700 na kuelekea kaskazini kuelekea Rutshuru, kampeni ya kuajiri kwa nguvu ilianza. HRW, ambayo ilifanya mahojiano yapatao 200 na wafungwa wa zamani, inaelezea kampeni hii kama ya kimfumo.

Askari wa Jeshi la Kongo (FARDC), maafisa wa polisi, watumishi wa umma, na raia wa kawaida walikusanywa katika vitongoji, hospitali, na makanisa: wote walipelekwa kwa nguvu kwenye kambi za Rumangabo na Tshanzu, ambapo shirika hilo linakadiria kuwa mamia ya watu walifariki mnamo mwaka 2025. Makaburi ya halaiki yameripotiwa na mashahidi huko Rumangabo na picha za setilaiti.

FARDC pia inahusishwa

Hata hivyo, ripoti hiyo pia inaishtumu serikali ya Kongo kwa kuunga mkono makundi yenye silaha yanayohusika na unyanyasaji mkubwa. Ripoti hiyo inabainisha, miongoni mwa mambo mengine, uungaji mkono wa FARDC kwa waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR na baadhi ya makundi ya Wazalendo yanayoshutumiwa kwa vurugu, kufunga watu kiholela, na kuwany’ang’anya mali zao watu waliokimbia makazi yao karibu na Goma.

Kwa hivyo, HRW inatoa wito kwa Kinshasa kuacha kutoa msaada wowote kwa makundi haya na kuanzisha uchunguzi huru unaolenga pande zote za mzozo.

Kigali, kama AFC/M23, haijazungumzi chochote kuhusiana na madai hayo, Human Right Watch pia inasema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *