
Rais wa Cuba atangaza mageuzi mapya ya kiuchumi ili kukabiliana na mzingiro wa kijinai wa Marekani
Mapendekezo hayo yaliyozinduliwa jana Ijumaa yanalenga kurekebisha uchumi wa kisiwa hicho na kufafanua tena nafasi ya Cuba katika soko la dunia.
Huku serikali ya Donadl Trump ikishadidisha hatua dhidi ya Cuba; serikali ya Havana inayoongozwa na Chama cha Kikomonisti inaratibu mnipango ya njia za ufumbuzi nje ya mtindo wake wa jadi wa kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutoa motisha kwa biashara za watu binafsi na kuvutia uwekezaji wa kigeni na kuingiza nchini teknolojia ya nishati jadidika.
Rais wa Cuba amesema katika mkutano na waandisi wa habari kwamba mapendekezo yaliyozinduliwa jana kwa ajili ya mageuzi mapya ya kiuchumi nchini humo yanatazamiwa kufafanua mkakati wa nchi hiyo wa kujibu sera kali kikamilifu ya serikali ya Marekani dhidi ya Cuba.
Rais wa Cuba Miguel Díaz-Canel amesema suala wanalopasa kujadili hivi sasa ni namna ya kukabiliana na kuzishinda changamoto hizo. Amesema Marekani haiwezi kupuuza ukweli kwamba, baada ya mashinikizo yake ya kiwango cha juu ya serikali ya Cuba lakini mapinduzi yapo yapo na nchi inaendelea kufanya kazi.
Rais Diaz- Canel ameongeza kuwa: Marekebisho hayo pia yatapanua ushiriki wa kiuchumi wa watu binafsi kutoka nje. Pia ameunga mkono suala la Wacuba wanaoishi nje ya nchi kuwekeza nchini.
Rais wa Cuba pia amesema serikali yake inataka kujitegemea nchi hiyo kwa upande wa chakula kupitia kuhimiza masoko ya ndani ya kilimo na kupanua upatikanaji wa fedha za kigeni kupitia kubadilishana masoko.