Mwendesha mashtaka ameuawa siku ya Jumapili, Juni 14, katika shambulio lililotokea katika mji wa bandari magharibi mwa Ecuador, ngome ya makundi kadhaa ya biashara ya dawa za kulevya, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imetangaza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Shambulio baya” katika mji wa pwani wa Manta, katika mkoa wa Manabí, limemlenga Gloria Bravo, ambaye alikuwa anafanya kazi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu iliyo karibu, ofisi hiyo imeongeza, ikilaani vikali shambulio hilo. Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kwamba dada yake hakimu, ambaye alikuwa naye wakati wa shambulio hilo, pia ameuawa.

Gloria Bravo alikuwa mwendesha mashtaka kwa miaka 15 na alikuwa amechunguza kesi kadhaa za uhalifu uliopangwa katika eneo hilo. Alipewa jukumu la kuchunguza mkasa wa moto wa hivi karibuni ulioharibu takriban boti 35 katika bandari ya uvuvi huko Manta, tukio ambalo hali yake bado haijathibitishwa na mamlaka.

Manta ni moja ya ngome kuu za kundi la wahalifu la Los Choneros. Kiongozi wake, maarufu kama Fito, alikamatwa na kupelekwa Marekani mwaka jana, ambapo anakabiliwa na mashtaka ya biashara haramu ya dawa za kulevya na silaha. Jiji hilo ni mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini Ecuador, nchi ambayo 70% ya kokeni kutoka kwa majirani zake, Colombia na Peru, wazalishaji wakuu wa dawa hii duniani, husafirishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *