Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili katika nafasi mbalimbali za umma, akimteua Nolasco Kipanda kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma na Balozi Modest Mero kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Jumanne Juni 23, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu.

Kabla ya uteuzi huo, Kipanda alikuwa akihudumu kama Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Taasisi katika Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Katika nafasi hiyo mpya, Kipanda anatarajiwa kusimamia majukumu ya kiutawala na kiutendaji ya Tume ya Utumishi wa Umma, ambayo ina jukumu la kusimamia masuala mbalimbali yanayohusu utumishi wa umma nchini.

Katika uteuzi mwingine, Rais Samia amemteua, Balozi Modest Mero kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, akichukua nafasi ya Profesa Saida Yahya Othman ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.

Balozi Mero anaingia katika nafasi hiyo wakati Chuo Kikuu Mzumbe kikiendelea na jukumu la kuimarisha elimu ya juu, utafiti na mchango wake katika maendeleo ya taifa.

Endelea kufuatilia Mwananchi…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *