
Umoja wa Mataifa umesema kuwa mlipuko wa virusi vya Ebola huenda ukaligharimu bara la Afrika kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.6 pamoja na maelfu ya ajira na pengine kusababisha mzozo wa kimaendeleo kwenye bara hilo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti ya tathmini iliyofanywa na shirika la umoja wa mataifa kuhusu maendeleo, imesema madhara ya janga hili yanakwenda nje ya sekta ya afya na lisipodhibitiwa hasara itakuwa kubwa zaidi.
Ikiwa mlipuko huu unaohusishwa na virusi vya Bundibugyo, hautadhibitiwa ndani ya DRC, utagharimu bilioni moja ya mapato ya kitaifa ya DRC, ripoti imeonesha.
Wataalamu wanasema licha ya kuwa nchi ya Uganda imeripoti idadi ndogo ya wagonjwa wa Ebola, kuna uwezekano mkubwa ukaenea kwenye nchi jirani ya Sudan Kusini na nchi nyingine za ukanda.
Aidha ripoti imeongeza kuwa nchini DRC watu zaidi ya milioni moja watatumbukia kwenye umaskini hata kama janga hili litadhibitiwa.
Kwa mujibu wa shirika lka maendeleo la umoja wa Mataifa, UNDP, mikakati ya kudhibiti msambao imeathiri biashara ,usafiri na shughuli za kiuchumi na kuweka shinikizo kwenye maisha ya wengi nchini DRC na nchi jirani.