Mtandao wa Madaktari wa Sudan leo umeripoti kuwa shambulio la ndege zisizo na rubani lililofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) limeua raia 10, wakiwemo wanawake watano kutoka familia moja, katikati mwa Sudan walipokuwa wakieleke harusini.

Mtandao huo umesema katika taarifa uliyoitoa leo kwamba wahanga wa hujuma hiyo ya walikuwa wakisafiri katika barabara ya Assadirat magharibi mwa mji wa Omdurman wakati walipolengwa na shambulio la ndege isiyo na rubani ya wanamgambo wa RSF. Ndege hiyo iliipifa gari ya raia na kusababisha kuwaka moto na kuuwa abiria wote katika gari hiyo.

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umelitaja shambulio hilo la RSF kuwa “ukiukaji mkubwa” wa sheria za kimataifa za kibinadamu, ukisema kuwa shambulio hilo llimefanywa kwa makusudi kwa kutumia ndege isiyo na rubani kwa kuwalenga raia wa kawaida.

Aidha umetoa wito ukitaka kushinikizwa uongozi wa RSF kuhusu kuwalenga raia kwa makusudi kinyume na sheria za kimataifa na kanuni za kibinadamu.

Sudan imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kuwania madaraka tangu mwezi Aprili 2023, jeshi la nchi hiyo na wanamgambo wa RSF. Mzozo huo umesababisha mojawapo ya majanga mabaya zaidi ya binadamu duniani, na kusababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu pamoja na kupelekea karibu watu milioni 13 kuwa wakimbizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *