Askofu wa Kanisa la Zanzibar International Christian Centre (ZICC), Dickson Kaganga amesema viongozi wa kisiasa wa pande mbili za Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo wameweka mbele mustakabali wa nchi kuliko maslahi binafsi, jambo lililowezesha kufikiwa kwa maridhiano ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani Zanzibar.
Askofu Kaganga amesema hayo leo Julai 9, 2026, alipokuwa akiongoza sala katika hafla ya kushuhudia tamko la pamoja la maridhiano ya kisiasa kati ya vyama hivyo viwili, iliyofanyika Ikulu, Zanzibar.
“Maridhiano haya yakalete tija kwa wananchi, maendeleo na ustawi wa kijamii,” amesema.
(Feed generated with FetchRSS)