Mapigano mapya kati ya Iran na Marekani yamezuka saa chache kabla ya mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, huku Tehran ikidai kushambulia maeneo yanayohusishwa na washirika wa Marekani katika ukanda wa Ghuba.

Iran imesema hatua hiyo ni majibu ya mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya maeneo mbalimbali nchini humo, huku Washington ikithibitisha kuendesha operesheni za kijeshi dhidi ya maeneo ya kijeshi ndani ya Iran.

Mvutano huo umeendelea katika siku ya pili ya mashambulizi ya anga ya Marekani, ambapo Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) imesema vikosi vyake vinaendelea kutekeleza operesheni dhidi ya maeneo kadhaa ya kijeshi nchini Iran.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *