#HABARI: Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetenga kiasi cha Sh.Milioni 432 kujenga kituo cha umahili taalumu kitakacho fahamila kama Edward Jonas Mpogolo Center for Excellence Capacity Building.
Hayo yameelezwa katika hafla ya utangazaji matokeo ya mitihani ya ndani na utoaji wa tuzo kwa wanafunzi na shule za sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani hiyo kwa kidato cha kwanza, pili, tatu na kidato cha sita, jiji Dar es Salaam.
Katika tuzo hizo Shule za Sekondari zilizofanya vibaya nazo zilikabidhiwa vinyago maalumu vya mpingo kwa lengo la kuleta hamasa kuleta matokeo mazuri kwa mwaka ujao.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema mkakati huo ni katika kuboresha sekta ya elimu ni kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Na kutekeleza maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha miundombinu ya elimu na ubora wa elimu itakayo mwezesha mhitimu kupata taaluma yenye tija.
Amesema Jiji la Dar es Salaam linaendelea na ujenzi wa Sekondari za ghorofa zenye vifaa vya kisasa,vitabu, kuimarisha nidhamu na uwajibikaji, matumizi ya teknolojia na kutekeleza mkakati wa kufuta ufaulu wa daraja sifuri na la nne.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amesema kituo hicho kitakapokamilika kitasaidia kuboresha usimamizi wa mitihani, umahili wa walimu na kutengeneza mfumo kama ya Baraza la Mitihani la Taifa (NACTE) kwaajili ya mitihani ya ndani.
Naye Ofisa Elimu Sekondari wa Jiji la Dar es Salaam,Mussa Ally, amesema hafla hiyo ya utoaji tuzo ni baada ya matokeo ya mitihani ya ndani ya Halmashauri iliyoratibiwa na kamati maalumu iliyoundwa nia ikiwa ni kupandidha ufaulu wa ndani kwa lengo la kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
@capitaldigitaltanz
(Feed generated with FetchRSS)