Kadri Kombe la Dunia 2026 linavyoelekea hatua za mwisho, baadhi ya klabu zimeendelea kutawala kupitia kiwango bora cha wachezaji wao wanaowakilisha timu za taifa.
Real Madrid ndiyo inaongoza kwa mchango mkubwa zaidi, huku wachezaji wake wakifunga jumla ya mabao 17. Mchango huo umetokana na nyota kama Kylian Mbappé (8), Jude Bellingham (6), Vinícius Jr (4) na Arda Güler, jambo lililoifanya klabu hiyo kuwa kinara wa mashindano.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Bayern Munich na Paris Saint-Germain (PSG), ambazo kila moja wachezaji wake wamefunga mabao 12. Kwa Bayern, Harry Kane ndiye kinara, huku PSG ikinufaika na kiwango bora cha Ousmane Dembélé pamoja na nyota wengine waliotawanya mabao kwa timu zao za taifa.
Zifuatazo ni Arsenal, Manchester United, Sunderland, Crystal Palace na Inter Miami, ambazo kila moja imechangia mabao 8 kupitia wachezaji wake walioko kwenye Kombe la Dunia.
Takwimu hizi zinaonyesha jinsi klabu kubwa duniani zinavyoendelea kuzalisha na kuendeleza wachezaji wanaong’ara kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka duniani.

(Feed generated with FetchRSS)