Wakati majina mengi yakitawala mijadala ya Kombe la Dunia 2026, Jude Bellingham ameendelea kuandika historia kimya kimya kwa kuibeba England katika mechi muhimu.

Kiungo huyo wa Real Madrid tayari amefunga mabao 6 kwenye mashindano haya, huku pia akitoa asisti 1, na kuwa mmoja wa wafungaji bora wa Kombe la Dunia.

Bellingham alianza kung’ara hatua ya mtoano alipofunga mabao mawili dhidi ya Mexico na kuiwezesha England kushinda 3-2 na kutinga robo fainali. Kisha akafanya hivyo tena kwenye robo fainali dhidi ya Norway, akifunga mabao yote mawili yaliyoiwezesha England kushinda 2-1 baada ya muda wa nyongeza na kutinga nusu fainali.

Mabao yake ya maamuzi yamekuwa sababu kubwa ya England kufika hatua ya nusu fainali, huku wengi wakimtaja kama mmoja wa wachezaji bora wa Kombe la Dunia 2026. Akiwa bado na umri wa miaka 23 pekee, Bellingham anaendelea kuthibitisha kuwa ni mchezaji wa mechi kubwa na tegemeo muhimu la England.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *