Mwanamitandao na mkufunzi wa mazoezi kutoka Marekani, Ashton Hall, Ashton Hall amemzawadia gari mtayarishaji wa maudhui kutoka Rwanda, Ashton Small, Kagarara anayejulikana pia kwa jina la Kagarara.

Ashton Small, ambaye jina lake halisi ni Enock Uwizeye, alipata umaarufu kupitia video zake za kuiga mtindo wa mazoezi na maisha wa Ashton Hall. Video hizo zilivutia mamilioni ya watazamaji na hatimaye zikamfanya Hall kuvutiwa na ubunifu wake.

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza nchini Ghana wakati wa ziara ya Ashton Hall barani Afrika. Baada ya kushirikiana kutengeneza maudhui, Hall alimzawadia Small gari kama ishara ya kuthamini juhudi, ubunifu na mchango wake katika ulimwengu wa uundaji wa maudhui.

Tukio hilo limepokelewa kwa furaha na maelfu ya mashabiki mitandaoni, huku wengi wakilisifu kama mfano wa kuthamini vipaji na kuhamasisha vijana kuendelea kutumia ubunifu wao kufikia mafanikio.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *