
Ingawa Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch linadai kwamba angalau wahamiaji 58 wa Ethiopia waliohukumiwa kifo nchini Saudi Arabia wanakabiliwa na hukumu ya kifo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia inabainisha kuwa inashiriki kikamilifu. Addis Ababa inaweka mbele msamaha wa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia uliotolewa kwa raia 1,971 wa Ethiopia na inadai kuendelea na juhudi zake za kidiplomasia na Riyadh.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Angalau Waethiopia kumi na wawili waliuawa mwaka huu nchini Saudi Arabia, kulingana na Human Rights Watch. Shirika hilo lisilo la kiserikali linasema kwamba wafungwa wengine 58 bado wanakabiliwa na hukumu ya kifo, hasa kwa biashara haramu ya dawa za kulevya.
Wafungwa hao wanashikiliwa Khamis Mushait, karibu na mpaka na Yemen. Miongoni mwao ni watu kadhaa wanaojaribu kuhamia Saudi Arabia ambao wanadai kusafirisha vifurushi vya wasafirishaji haramu bila kujua yaliyomo.
Kulingana na Joey Shea, mtafiti wa Human Rights Watch aliyebobea kuhusu Saudi Arabia, hawajapata fursa ya kujitetea: “Wafungwa hawa walisikilizwa tu mara hache kwa wakatimmoja, mara nyingi kupitia mkutano wa video, uliyodumu chini ya dakika 10, ambapo wanaume hawa hawakuwa na uwakilishi wa kisheria, hata wakalimani, na mara nyingi hawakuarifiwa kuhusu mashtaka dhidi yao. Wakati wa vikao hivi, wanaume hawa walilazimishwa kusaini hati ambazo hawakuzielewa.” “
Saudi Arabia imekuwa ikipigana vita dhidi ya dawa za kulevya kwa miaka kadhaa, na sera hii inaambatana na ongezeko la matumizi ya adhabu ya kifo. Nchi hiyo imevunja rekodi yake ya idadi ya watu walionyongwa miaka miwili mfululizo. Wageni huathiriwa hasa katika visa hivi vya dawa za kulevya.
Mamlaka za Ethiopia zinadai kuhamasishwa. Lakini kulingana na Human Rights Watch, hakuna dalili hadi sasa kwamba wafungwa 58 wanaokabiliwa na adhabu ya kifo wamepokea msaada wowote kutoka kwa serikali yao.”