
Spika wa Bunge la tiaf la Senegal, Ousmane Sonko, ambaye alikuwa kiongozi wa upinzani nchini Senegal na Waziri Mkuu mfululizo kabla ya kuwa Spika wa Bunge la taifa, amemkosoa vikali mshirika wake wa zamani na Mkuu wa Nchi wa sasa mnamo Julai 12, 2026, huko Touba.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff
“Raia wa Senegal wanapaswa kujua kwamba kwa vyovyote vile hawana wasiwasi na Bassirou Diomaye Faye,” alisema Ousmane Sonko, akitishia kuiangusha serikali “ikiwa inahitajika” kutokana na wingi wake wa wabunge. Kinachojadiliwa, haswa, ni kutokubaliana kuhusu usimamizi wa uhuru wa nchi.
Nchini Senegal, makubaliano ya amani kati ya mkuu wa nchi na mshirika wake wa zamani na Waziri Mkuu wa zamani yalikuwa ya muda mfupi: wakati akizindua makao makuu ya chama cake cha PASTEF, katika jiji takatifu la Touba Jumapili jioni, Ousmane Sonko alitoa shambulio kali dhidi ya Bassirou Diomaye Faye na maamuzi yake ya kisiasa.
Spika wa sasa wa Bunge la taifa, ambaye chama chake kinaongoza idadi kubwa ya viti bungeni, alitishia kuipindua serikali kupitia hoja za kutokuwa na imani.
Ousmane Sonko, ambaye alikuwa ameahidi kutoizuia serikali ya sasa, amebadilisha msimamo wake na kutangaza kuwa tayari kuipindua timu iliyo madarakani “ikiwa inahitajika.”
Kiongozi wa PASTEF anabaini kwamba Waziri Mkuu wa sasa Ahmadou Al Aminou Mohamed Lô na Bassirou Diomaye Faye wakataa mazungumzo ya mikataba ya kimkakati na mashirika ya kimataifa kwa ajili ya usimamizi wa maliasili, haswa fosfeti.
“Tuna ushujaa wa kukabiliana naye,” alisema Ousmane Sonko, akiishutumu serikali kwa kubomoa kile ambacho imefanya ili kuhifadhi mazingira ya biashara.
Spika wa Bunge, ambaye alikuwa mzungumzaji mkuu mnamo Julai 12, alimshutumu Bassirou Diomaye Faye kwa kutanguliza matarajio yake ya kisiasa kwa kuunda chama chake kuliko maslahi ya raia wa Senegal, akizungumzia, miongoni mwa mambo mengine, deni la umma na ukosefu wa mpango na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). “Raia wa Senegal wanapaswa kujua kwamba kwa vyovyote vile hawana wasiwasi na Diomaye Faye,” Ousmane Sonko aliwaambia wafuasi wake huko Touba.
“Ni rais gani anayeweza kumudu kuwa na muda wa kuwaita watu kuanzia asubuhi hadi usiku kwenye Ikulu ya Jamhuri ili kuunda chama kipya cha siasa wakati ambapo tuna deni ambalo halijaweza kulipwa, wakati hakuna mpango wowote na IMF, wakati msimu wa mvua umejaa kutokuwa na uhakika, wakati mambo yanapozidi kuwa mabaya katika sekta zote za maisha ya kijamii na kiuchumi?” aliongeza mkuu huyo wa zamani wa serikali, kabla ya kumalizia, bado akizungumza kwa Kiwolof, alisema: “Tutamkabili. Tuna Bunge, kwa hivyo tuna njia za kumkabili.”
Spika wa Bunge kwa hivyo anajiweka kama kiongozi mkuu wa upinzani nchini na kumtuhumu Mkuu wa Nchi kwa kusaliti mradi wa uhuru ambao alichaguliwa, na hivyo kuanzisha shambulio jipya la mawasiliano ya kisiasa.
Waziri Mkuu Ahmadou Al Aminou Mohamed Lô hakusita kujibu matamshi ya Ousmane Sonko. “Kujaribu kufanya uzalendo kuwa ukiritimba wa upande mmoja, haswa, ni sawa na kuusaliti,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Kama ukumbusho, mnamo Julai 9, Baraza la Katiba la Senegal lilibatilisha rasimu iliyopitishwa na Bunge wiki iliyopita ya kurekebisha usawa wa madaraka kati ya serikali kuu na bunge, huku kukiwa na mzozo kati ya rais wa nchi hiyo na rais wa Bunge.
Baada ya miezi kadhaa ya mvutano kati ya Bassirou Diomaye Faye na mshauri wake wa zamani, Ousmane Sonko, ambaye alifukuzwa kutoka wadhifa wake kama Waziri Mkuu mnamo Mei 22. Lakini Ousmane Sonko alirudi nyuma na kuchaguliwa Mei 26 kama spika wa Bunge la taifa, ambalo kwa kiasi kikubwa linaongozwa na chama chake, PASTEF.