
Wanafunzi wa shule 20 na mtu mmoja mzima, wamepoteza maisha, nchini Uganda baada ya Basi, walilokuwa wanasafiria kuhusika kwenye ajali ya barabarani, katika Wilaya ya Kapchorwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ajali hiyo imetokea Alhamisi usiku, wakati wanafunzi hao kutoka Shule la msingi ya King David Junior kutoka jijini Kampala, walipokuwa wanarejea shuleni wakitokea kwenye ziara ya masomo katika kivutio cha Sipi Falls.
“Dereva alipoteza mwelekeo na kugonga jiwe kubwa kando ya barabara na kubingiria,” ripoti ya Polisi imesema.
Aidha, ajali hiyo imesababisha majeraha ya watu wengine watatu.
Nchini Uganda, ajali za barabarani hutokea mara kwa mara nchini Uganda, kwa sababu ya uendeshaji wa kasi na hali mbaya ya Barabara.
Mwezi Oktoba mwaka uliopita, abiria 46 walipoteza maisha katika ajali nyingine ya barabarani katika nchi hiyo ambayo hupoteza watu karibu elfu tano kila mwaka.