Washington imetangaza usiku wa Alhamisi, Julai 16, kuamkia Ijumaa, Julai 17, kuwa imefanya mashambulizi mapya dhidi ya Iran “ili kudhoofisha zaidi uwezo wa kijeshi wa Iran,” hasa katika Kisiwa cha Qeshm na karibu na Bandar Abbas, ambako kunapatikana  bandari kubwa zaidi ya Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Tehran imeripoti mashambulizi kadhaa kwenye madaraja, uwanja wa ndege, na kituo cha treni, na kuua watu wasiopungua saba. Iran imejibu kwa kuanzisha mashambulizi dhidi ya vituo vya Marekani katika nchi za Ghuba.

Katika siku ya sita ya mashambulizi yake dhidi ya Iran, Washington inasema inataka “kupunguza zaidi uwezo wa kijeshi” unaotumika dhidi ya meli za kibiashara katika Mlango wa Hormuz. Jeshi la Marekani limeema kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba lilishambulia “maeneo kadhaa ya kijeshi ya Iran, ikiwa ni pamoja na maeneo ya ufuatiliaji wa pwani na ulinzi wa anga, miundombinu ya vifaa vya kijeshi, na mitambo ya baharini” usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa.

Tehran, kwa upande wake, imeishutumu Washington kwa kulenga maeneo ya raia, ikiwa ni pamoja na madaraja mawili katika eneo la Bandar Khamir, na kuua watu saba, pamoja na kituo cha treni huko Bandar Abbas na Uwanja wa Ndege wa Iranshahr. Jamhuri ya Kiislamu imerudia tishio lake la kulipiza kisasi kwa kushambulia “miundombinu yote katika eneo la Ghuba” ikiwa “Marekani itashambulia miundombinu ya Jamhuri ya Kiislamu.”

Muda mfupi baada ya mashambulizi ya Marekani, Tehran ilitangaza Ijumaa, Julai 17, kwamba itazindua mashambulizi mapya katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kituo cha amri cha Marekani huko Al-Tanf, Syria. Hii inakuja baada ya Iran kulenga vituo vya kijeshi vya Marekani huko Jordan kwa kutumia ndege zisizo na rubani siku ya Alhamisi, Julai 16, kulingana na televisheni ya serikali, kufuatia mashambulizi zaidi ya anga ya Marekani nchini Iran. Tehran pia inadai kushambulia vituo vya Marekani huko Bahrain na Kuwait mapema Ijumaa asubuhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *