Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, kulipiza kisasi damu ya Imam shahidi kutaendelea hadi kuondoka Marekani katika eneo hili na kuangamia utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mohammad Javad Haj Ali Akbari amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran katika Musalla wa Imam Khomeini na kubainisha kwamba, wananchi wa Iran wanajitambua kuwa wao ni waliii wa damu ya Imam Shahidi Ayatullah Ali Khamenei.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameeleza kuwa, uaminifu, upendo, subira na uimara wa wananchi wa Iran tangu mwanzo wa Uislamu hadi leo ni jambo la kuigwa na kusisitiza kwamba: “Mahudhurio na uwepo huu ulikuwa kama kura kubwa ya maoni ya kuhuisha ahadi ya uaminifu kwa malengo ya Mapinduzi, na pia ulikuwa ni kiapo cha utii kwa kiongozi wetu mpendwa kuliko uhai wetu.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Mohammad Javad Haj Ali Akbari amesema, kipengele maalumu cha tukio hili kubwa la kishujaa kilikuwa neno moja tu: ‘kisasi’.

Kisasi ni matakwa ya wote, ya hakika na ya dhati, yanayotokana na busara na yanayozingatia misingi iliyo wazi ya Sheria Tukufu, ambapo Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 179 ya Surat al-Baqarah: “Na mna uhai katika kulipiza kisasi, enyi wenye akili ili msalimike.”

Aliongeza kusema: “Adui anapaswa kufahamu kwamba hili ni jambo lenye msingi kamili wa kisheria, wa haki na lenye uzito. Hili si ombi linalotokana na hisia tu, bali pia lina lengo la kuzuia na kuleta tahadhari (kuzuia kurudiwa kwa vitendo kama hivyo).

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Haj Ali Akbari, amesema kuwa mchakato wa kudhoofika ubeberu wa dunia unaoongozwa na Marekani umeanza na kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, mchakato huu umechukua kasi wakati wa vita vya hivi karibuni, na Marekani imedhalilika mbele ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akizungumzia ukiukwaji wa makubaliano ya pamoja uliofanywa na Marekani Imamu wa muda wa Swala ya Ijumaa amesema:

“Marekani kwa mara nyingine tena imekiuka ahadi zake na, kwa kushambulia maeneo ya kusini mwa nchi, kambi za kijeshi, hospitali, madaraja, miundombinu, vituo vya mazingira na maeneo ya uvuvi, imefanya vitendo vya uhasama.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *