Mbunge wa Jimbo la Kwela ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ametaka watumishi wa umma wote wanaodaiwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za mradi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mfinga kufikishwa mahakamani haraka baada ya kubainika kuwepo kwa viashiria vya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Sangu ameeleza kuwa kati ya Shilingi milioni 220.1 zilizotolewa kwa mradi huo tangu Julai 2025, tayari Shilingi milioni 212.9 zimetumika lakini ujenzi bado haujakamilika jambo ambalo linaibua maswali kuhusu uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *