Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa kulinda amani na usalama wa nchi, akisema ndio msingi wa maendeleo na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika miradi ya kimkakati.

Akizungumza leo Julai 20, 2026 wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Tabora–Kigoma pamoja na meli nne za mizigo katika Ziwa Tanganyika, Rais Samia alisema uwekezaji katika miundombinu unagharimu fedha nyingi hivyo unapaswa kulindwa.

“Nipende kusisitiza suala la amani, usalama na maendeleo ya nchi yetu, uwekezaji huu unagharimu fedha nyingi sana,” alisema Rais Samia.

Alisema Watanzania wanapaswa kuwa na mtazamo wa kuweka usalama mbele, akieleza kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa mazingira salama.

“Niwaombe sana wote kuwa na itikadi ya usalama kwanza na maendeleo yetu, bila usalama hakuna maendeleo,” amesema.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *