Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mheshimiwa Deus Sangu amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuimarisha programu ya mafunzo ya uanagenzi kama mkakati wa kuwajengea vijana stadi za kazi zitakazowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine, hatua inayolenga kuongeza fursa za ajira na kukuza uchumi wa Taifa.

Waziri Sangu alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26 Serikali, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewezesha vijana 5,746 kupata mafunzo ya uanagenzi katika vyuo 46 nchini huku ikigharamia ada za mafunzo, bima ya afya na nauli za mafunzo kwa vitendo.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *