John Stones

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 3

Arsenal wanazingatia kumsajili beki wa England mwenye umri wa miaka 32, John Stones, kwa uhamisho wa bure iwapo itabainika kuwa jeraha la beki wa Ufaransa mwenye miaka 25, William Saliba, litamweka nje kwa muda mrefu.

Chelsea wamefanya mazungumzo rasmi na Crystal Palace kuhusu kumsajili beki wa Ufaransa Maxence Lacroix, huku Palace wakimthaminisha mchezaji huyo wa miaka 26 kwa takribani pauni milioni 55.

Hull City wako kwenye mazungumzo na Aston Villa kuhusu uhamisho wa winga wa Jamaica mwenye miaka 28, Leon Bailey.

Meneja mpya wa Fulham, Alvaro Arbeloa, anataka kusajili wachezaji wawili kutoka klabu yake ya zamani ya Real Madrid, akiwemo winga wa Argentina mwenye miaka 18 Franco Mastantuono na mshambuliaji wa Hispania mwenye miaka 22 Gonzalo Garcia.

Winga wa England mwenye miaka 23 wa Bologna, Jonathan Rowe, bado yupo kwenye orodha za usajili za Aston Villa na Chelsea.

Hull City wanakaribia kukamilisha usajili wa mlinzi wa kushoto wa zamani wa Newcastle, Matt Targett, mwenye miaka 30, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Newcastle msimu huu wa kiangazi.

Matt Targett

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool wako tayari kuingia kwenye mbio za kumsajili kiungo wa Ufaransa wa Roma mwenye miaka 25, Manu Kone, huku Manchester United pia wakimuwania.

Aston Villa wamefanya mazungumzo na Chelsea kuhusu uwezekano wa kuwasajili washambuliaji Nicolas Jackson na Alejandro Garnacho msimu huu wa kiangazi.

Mshambuliaji wa Ureno wa AC Milan mwenye miaka 27, Rafael Leao, angependelea kuhamia Ligi Kuu ya England badala ya Uturuki, huku Aston Villa ikitajwa kuwa moja ya klabu zinazoweza kumsajili.

Rafael Leao

Chanzo cha picha, Getty Images

Lazio wanamuwania beki wa DR Congo wa West Ham mwenye miaka 28, Aaron Wan-Bissaka, ambaye pia yupo kwenye orodha ya chaguo za Arsenal.

Kipa namba moja anayelengwa na Juventus ni kipa wa Aston Villa na Argentina mwenye miaka 33, Emiliano Martinez. Klabu hiyo ya Serie A pia inamfuatilia kipa wa Fiorentina na Hispania mwenye miaka 35, David de Gea.

Everton wanaweza kushindana na Inter Milan katika mbio za kumsajili beki wa England wa Tottenham mwenye miaka 25, Djed Spence.

Liverpool wanataka kumsajili beki wa kushoto wa Sweden mwenye miaka 24, Daniel Svensson, kutoka Borussia Dortmund, lakini wanaweza kukumbana na ushindani kutoka Arsenal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *