ARUSHA: WAGONJWA zaidi ya 21,000 wamepatiwa matibabu katika kambi ya tiba ya siku saba iliyoandaliwa na kuratibiwa na Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Paul Makonda kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kati yao wagonjwa 982 wamegundulika kuwa na magonjwa mpya bila wao kujijua.

Hayo yalisemwa na Makonda wakati akifunga kambi hiyo na kusema kuwa katika magonjwa matatu ikiwemo Kansa ,moyo na sukari wagonjwa 982 walikutwa na magonjwa mapya baada ya kupimwa afya na wao hawakuwa wanajua kama wana ugonjwa huo.

Makonda alisema katika ugonjwa wa sukari waligonjwa 6,297 walipimwa na wagonjwa 503 walikutwa na ugonjwa huo,wagonjwa wa kansa 836 walipimwa na wagonjwa 18 walikutwa na dalili za ugonjwa huo na ugonjwa wa Moyo walipima wagonjwa 1,665 na 461 walibainika na ugonjwa huo.

Alisema kwa mujibu wa madaktari bingwa na wabobezi walisema kuwa wagonjwa wote waliokutwa na ugonjwa ama dalili za ugonjwa wanaweza kupata tiba iwapo wataanza mara moja matibabu na yeye atahusika kwa namna moja ama nyingine kuwatibu wagonjwa hao kwa kuwa walipata matibabu katika kambi hiyo.

Waziri Mkonda alisema kambi ililenga kwa watu wasiokuwa na uwezo kupima afya na wagonjwa kupata matibabu na isingewezekana kuongeza siku kwa kuwa Madaktari Bingwa na Wabobezi waliokuwa waliokuwa wakitoa huduma kwa muda huo wanahitajika katika maeneo yao ya kazi hivyo sio rahisi kuongeza siku tena.

Alisema madaktari waliokuwa wakitoa huduma katika kambi ya matibabu wamefanikiwa kutoa matibabu kwa wakazi wa Jiji la Arusha na nje ya jiji kwani wote ni watanzania na walikuwa na umuhimu wa kupata matibabu kama wagonjwa wengine.

Waziri Makonda alisema wingi wa wagonjwa ulifanya kila daktari kuhudumia wagonjwa zaidi ya watatu kwa magonjwa tofauti na kila siku wagonjwa 3,600 walihudumiwa katika kambi hiyo ambayo itakuwa ikifanyika kila mwaka ndani ya Jiji la Arusha.

“Kambi hii ni muhimu kwa afya ya wakazi wa Jiji la Arusha na amewataka wakazi wa Arusha kumwombea ili aweze kutimiza malengo yake ya kuwatumikia wakazi wa Jimbo hilo” Alisema Makonda

Naye, Mkazi wa kata ya Sekei Jijini Arusha,Asha Mohamed alisema kuwa kambi hiyo ni muhimu sana kufanyika kwani watanzania hawana tabia ya kupima afya mara kwa mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *