
Wanajeshi 50 wa Mali wameripotiwa kuuawa katika shambulio la kushtukiza lililotekelezwa wikendi iliopita na wapiganaji wa Tuareg wakishirikiana na wale wakijihadi kaskazini mwa mji wa kimkakati wa Anefis.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shambulio dhidi ya msafara wa jeshi la Mali uliokuwa ukitoka Anefis lilitokea mwishono mwa wiki iliyopta, na linafuatia majuma kadhaa ya mapigano kila upande ukijaribu kuwa na udhibiti wa eneo hilo.
Mwanzoni mwa mwezi Julai, wapiganaji wa Tuareg na wanajihadi wenye uhusiano na mtandao wa Al Qaeda, JNIM, waliuteka mji huo na kuzizunguka kambi za jeshi la Mali na wapiganaji mamluki wa Urusi.
Kwa mujibu wa vyanzo toka jeshi la Mali, vinasema idadi ya wanajeshi waliouawa huenda ikaongezeka huku vikithibitisha uwepo wa majeruhi, huku wanajeshi wa Urusi ambao walikuwa wamefika mji wa Gao wakiwa hawajapata maafa yoyote kutokana na shambulio hili.
Nchi ya mali imekuwa ikiongozwa na wanajeshi tangu yalipofanyika mapinduzi mfululizo mwaka 2020 na 2021, na tangu wakati huo jeshi limekuwa likikabiliwa na tishio toka kwa waasi wa Tuareg na wanajihadi wa kiislamu wa Kundi la JNIM Kaskazini mwa nchi hiyo.